Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, amewakaribisha ofisini kwake viongozi wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), walipomtembelea kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya SHIMIWI 2026.
Michezo hiyo inatarajiwa kufanyika mkoani Kilimanjaro, ikiwakutanisha timu kutoka Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa kutoka kote nchini, ikishirikisha takribani michezo 10.
Wizara, Idara na Taasisi zinazotarajia kushiriki zinahimizwa kukamilisha usajili wa timu na wachezaji wao kupitia mfumo huu, na kulipa ada husika kwa wakati ili kuwa na sifa ya kushiriki.



