
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, akiwakaribisha ofisini kwake viongozi wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), walipomtembelea kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya SHIMIWI inayotarajiwa kuanza tarehe 19 Septemba na kumalizika Oktoba 7, 2026 mkoani hapo.