Mafunzo ya Viongozi, Walimu wa Michezo, Madaktari, Waratibu na Maafisa Michezo yamefanyika mkoani Morogoro tarehe 25 hadi 27 Februari 2026 kwenye Ukumbi wa Mbaraka Mwishehe.
Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo wasimamizi wa michezo katika Wizara, Idara na Wakala za Serikali ili kuboresha usimamizi, usalama na ubora wa mashindano ya SHIMIWI.
Ujenzi huu wa uwezo ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea Michezo ya SHIMIWI 2026, huku ushiriki wa kitaalamu ukilenga kuinua viwango vya uendeshaji wa mashindano.







